Friday, November 19, 2010

Ya Peik, Mjengwa na Wanahabari kuhusu mafunzo ya ICT Arusha

Ya Peik, Mjengwa na Wanahabari kuhusu mafunzo ya ICT Arusha

NI takribani siku tano hivi, Vijana wa kazi ambao ni Waandishi wa habari wa Kanda ya Kaskazini (Nothern Zone) walikuwa katika darasa maalumu katika Jiji la Arusha wakijifunza ICT ili kwenda sambamba na wanataaluma wengine duniani.

Ilikuwa ni kuanzia Novemba 15 – 19 mwaka 2010,Majengo ya Summit Centre mjini Arusha ambapo kipo kituo cha Kompyuta ambalo ni tawi la Chuo kikuu cha Dar es Salaam (University of Dar es Salaam,Arusha Computer Centre) wanahabari walikuwa wakiumiza vichwa lakini wengine ilikuwa shida tupu!

Mada zilikuwa chini ya Mzungu Peik,raia wa Finland na Mwandishi wa Habari mkongwe wa kimataifa aliyebobea katika utangazaji upande wa Redio.

Ni hatua nzuri kwa wanahabari wetu lakini siamini na sitaki kuamini kama wote hizo Blogs zitakuwa active kwa muda wote.

Haya Misa Tanzania kazi kweni,Je! Mafunzo haya yataleta chachu?

No comments:

Post a Comment